Ali Omar amekuwa mvuvi kwa muda wa miaka 18 kisiwani Lamu, katika pwani ya Kenya. Zaidi ya hayo, ameshirikiana na wengine kutengeneza mifuko inayotokana na vitambaa vya Tanga, ambavyo vinatokana na vitambaa kuu kuu vinavyotumiwa katika boti za wavuvi baharini. Mifuko hiyo huuzwa kwa watalii na wenyeji wa Lamu.